Kicheko Fursa
Written by admin on June 21, 2025
Radio Kicheko inakupa fursa ya kutangaza au kudhamini kipindi kwa ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu. Unaweza kuwasiliana na wataalam wetu kwa namba +255 677 700 003 ili kupewa utaratibu.
Matangazo ya redio yamegawanyika katika mufungu kadhaa na ni muhimu kupata maelekezo sahihi ili uweze kufanya uamuzi sahihi kwako.
Aina ya kwanza ni matangazo mafupi yanayoitwa “jingles”. Haya ni matangazo ya sekunde kadhaa hadi dakika moja yakiwa na kionjo cha muziki wa kuanzia na kufunga.
Aina ya pili ni udhamini wa kipindi au baadhi ya vipindi. Kipindi kilichodhaminiwa kitarusha tangazo la mdhamini mwanzo na mwisho wa kipindi na katikati ya kipindi yatasomwa maelezo ambayo yanajulikana kitaalam kama “mention”.
Aina ya tatu ni kipindi maalum ambapo kinatengenezwa kipindi maalum chenye maudhui ya kuitangaza taasisi, bidhaa na huduma zake.
Kwa kukusikiliza kwa makini kile unachotaka kufanya wataalam wetu watakuelekeza njia bora na sahihi ya kufikia malengo yako.
Karibuni sana