Watangazaji Mahiri

Written by on June 30, 2019

Radio Kicheko Live inajivunia kujumuisha jopo la Waandishi na Watangazaji nguli wenye uzoefu wa miaka mingi katika tasnia ya habari na pia vijana wanaochipukia ambao wako tayari kujifunza na kujiendeleza.

Wanahabari wa Radio Kicheko Live wamepatikana baada ya kupitia mchakato mrefu wenye ushindani mkali ambapo walifanya mtihani wa mwanzo, na wale waliofaulu hatua hiyo ya mwanzo wakapatiwa mafunzo yaliyohitimishwa na mtihani mwingine.

Wanahabari waliofanikiwa kupenya hatua hiyo wakapewa mikataba ya ajira na kuanza mafunzo ya ndani ambayo ni endelevu. Mafunzo ya ndani yalianzia darasani kwa miezi kadhaa na baadae kuhamia katika vitendo na hatimae kwenye uzalishaji wa vipindi na habari.

Radio Kicheko Live imejizatiti kujenga timu ya wanahabari wenye nidhamu ya hali ya juu, wanaofanya kazi kwa weledi na ubunifu. Tunaamini kila atakayebahatika kusikiliza habari na vipindi vyetu ataona na kutambua mara moja tofauti na redio zingine.

Radio Kicheko Live inakaribisha taasisi na biashara na hata watu binafsi wenye matangazo kuwasiliana na idara yetu ya masoko kwa ajili ya kupatiwa utaratibu wa kutangaza au kudhamini vipindi.

Wote mnakaribishwa!

Tagged as

Continue reading

Current track

Title

Artist

Background