Kilimo Biashara

Written by on June 29, 2019

Sikiliza Radio Kicheko Live upate fursa ya kujifunza kilimo chenye tija na manufaa kibiashara.

Kilimo hai (organic farming), kilimo cha matone (drip irrigation), kilimo kisichotumia udongo (hydroponic irrigation), kilimo cha shamba kitalu (green house), nk

Aina zote hizi na zingine nyingi zinafundishwa na kuchambuliwa na wataalamu na pia wakulima na wajasiriamali ambao wanafahamu hali halisi na changamoto zilizopo ili kukupa wewe msikilizaji elimu na maarifa yaliyokamilika kuhusu kilimo biashara.

Kipindi cha Mtaalamu Wetu wa Kilimo ni kila Alhamisi kuanzia saa mbili na robo usiku na kurudiwa kila Ijumaa saa nane kamili mchana.

Radio Kicheko Live imejizatiti kujenga timu ya wanahabari wenye nidhamu ya hali ya juu, wanaofanya kazi kwa weledi na ubunifu. Tunaamini kila atakayebahatika kusikiliza habari na vipindi vyetu ataona na kutambua mara moja tofauti na redio zingine.

Radio Kicheko Live inakaribisha taasisi na biashara na hata watu binafsi wenye matangazo kuwasiliana na idara yetu ya masoko kwa ajili ya kupatiwa utaratibu wa kutangaza au kudhamini vipindi.

Wote mnakaribishwa!Continue reading

Current track

Title

Artist

Background