Kicheko Fursa

Written by on July 5, 2019

Radio Kicheko Live inakupa fursa ya kutangaza biashara yako popote pale ulipo kwa gharama nafuu kabisa. Wataalamu wetu wa masoko watakushauri namna bora ya kufikisha ujumbe wa biashara yako kwa wasikilizaji na kukusaidia kuongeza wateja.

Kicheko Fursa imegawanyika katika makundi yafuatayo:

COMMERCIAL – Radio Kicheko Live inatengeneza matangazo ya biashara kwa utaalamu wa hali ya juu kwa kuongeza vionjo na special sound effects ili kuyafanya yawe na mvuto wa kipekee. Matangazo haya huwa na urefu usiozidi dakika moja.

ADVERTORIAL – Radio Kicheko Live inatengeneza matangazo kupitia kipindi maalum kuhusu kazi au biashara yako kwa namna ambayo itawafanya wasikilizaji waielewe, waiamini, na kuipenda bidhaa yako. Kipindi cha namna hii huweza kuwa na urefu wowote na pia vinaweza kuwekwa katika mtiririko wa vipindi kadhaa ambavyo vitatangazwa katika siku tofauti.

CASUAL – Radio Kicheko Live inapokea na kusoma matangazo kama yanavyoletwa na Mhusika bila kuweka vionjo wala special sound effects zozote. Matangazo ya aina hii ni ya muda mfupi na gharama yake ni nafuu zaidi.

WAJASIRIAMALI – Radio Kicheko Live imetengeneza fursa maalum kwa wajasiriamali wadogo kutangaza shughuli na bidhaa zao kwa gharama nafuu sana wanayoweza kuimudu. Kwa gharama ndogo kabisa kila Mjasiriamali anaweza kutangaza bidhaa yake na kutoa namba zake za mawasiliano.

UPENDO ADVERTS – Radio Kicheko Live inatoa fursa ya matangazo ya kijamii kwa kila mtu anayetaka. Ni fursa maalum ya kuonyesha upendo kwa kuwapongeza uwapendao katika kumbukumbu muhimu kama Harusi, Birthday, Sendoff, Ubarikio, Graduation na pia matangazo na kumbukumbu za vifo.


Continue reading

Current track

Title

Artist

Background