Sasa Rasmi!

Written by on June 29, 2019

Radio Kicheko Live imepokea rasmi leseni ya utangazaji kwa redio kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Leseni hiyo ya miaka mitano ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi mwenza wa Radio Kicheko Live, Mrs Phlaviana Kavishe, huko Arusha tarehe 25 Juni 2019 na Kaimu Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, Ms Imelda Salum.

Radio Kicheko Live inarusha matangazo yake katika masafa ya MHz 91.1 na inasikika katika mikoa ya Kilimanjaro, baadhi ya sehemu za mikoa ya Arusha na Manyara. Vile vile inasikika baadhi ya sehemu za mpakani mwa Kenya kama Taveta.

Radio Kicheko Live imejizatiti kujenga timu ya wanahabari wenye nidhamu ya hali ya juu, wanaofanya kazi kwa weledi na ubunifu. Tunaamini kila atakayebahatika kusikiliza habari na vipindi vyetu ataona na kutambua mara moja tofauti na redio zingine.

Radio Kicheko Live inakaribisha taasisi na biashara na hata watu binafsi wenye matangazo kuwasiliana na idara yetu ya masoko kwa ajili ya kupatiwa utaratibu wa kutangaza au kudhamini vipindi.

Wote mnakaribishwa!


Continue reading

Current track

Title

Artist

Background