Kapu la Historia
Written by admin on June 29, 2019
Sikiliza Radio Kicheko Live upate fursa ya kujifunza historia ya nchi yetu, makabila, mila desturi na matukio muhimu ya kihistoria.
Wahenga walisema “Msahau kwao Mtumwa” na vile vile tunafahamu kuwa asiyekumbuka nyuma alikotoka mara nyingi huwa hana shukurani kwa sababu anakosa tathmini sahihi ya pale alipofikia.
Ni vyema wakati tunajitahidi kwenda mbele, kwenda na wakati, kutembea katika karne hii ya sayansi na teknolojia, vile vile tukumbuke tulikotoka, tukumbuke historia, pamoja na kuwapa heshima na kuwaenzi wale wote waliochangia hadi sisi tukafika tulipo na kuwa tulivyo.
Kipindi cha Kapu la Histori ni kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuanzia saa tano na nusu hadi saa sita kasorobo mchana.
Radio Kicheko Live imejizatiti kujenga timu ya wanahabari wenye nidhamu ya hali ya juu, wanaofanya kazi kwa weledi na ubunifu. Tunaamini kila atakayebahatika kusikiliza habari na vipindi vyetu ataona na kutambua mara moja tofauti na redio zingine.
Radio Kicheko Live inakaribisha taasisi na biashara na hata watu binafsi wenye matangazo kuwasiliana na idara yetu ya masoko kwa ajili ya kupatiwa utaratibu wa kutangaza au kudhamini vipindi.
Wote mnakaribishwa!